Baada ya Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 23 kupoteza mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki michuano ya Afcon kwa kufungwa bao 2-0 dhidi ya Burundi, kocha Bakari Shime ameibuka na kutoa neno la matumaini.
Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Bunjumbura ni wa kwanza na mchezo wa marudiano utapigwa Tanzania hali iliyomfanya Shime kuamini watapindua meza kibabe.
"Bado tuna nafasi ya kusonga mbele kwa kuwa ni mchezo wa kwanza, tumepoteza kutokana na kuzidiwa mbinu, mpira ni mchezo wa makosa, hivyo tunauwezo wa kupata matokeo tukiwa nyumbani, mashabiki watupe sapoti," alisema.
Ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele timu ya taifa itapaswa kupata ushindi wa mabao zaidi ya matatu ili kuweza kupenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment