Baada ya Emmanuel Okwi, kupata tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Ligi Kuu Bara, mshambuliaji mwezanke wa Simba Meddie Kagere amempongeza na kuahidi kuendelea kujituma.
Kagere alikuwa mchezaji wa kwanza kupata tuzo hiyo mwezi Agosti, baada ya kuwashinda Joseph Mahundi wa Azam FC na Ompar Mponda wa Kagera Sugar, lakini hivi karibuni TFF walimtangaza Okwi kama mchezaji bora wa mwezi Oktoba.
Kagere alisema kuwa anaona fahari mchezaji mwenzake akipata kile ambacho anastahili kutokana na juhudi zake ndani ya timu.
"Okwi amepata tuzo ya mchezaji bora hilo ni jambo zuri kwetu kwa kuwa linaleta nguvu ya kuendelea kujituma, kwa mambo aliyoyafanya amestahili kupewa hiyo tuzo kwani jiihada zake zimeonekana, kikubwa ni kuongeza zaidi juhudi," alisema Kagere.
Okwi amepewa tuzo hiyo baada ya kuwazidi aliofika nao fainali ambao ni pamoja na Yahya Zayd wa Azam na Eliud Ambokile wa Mbeya City baada ya kufanikiwa kufunga mabao 7 katika mechi 4 na kusaidia kupatikana pointi 12.
0 COMMENTS:
Post a Comment