Mshambuliaji wa Mbeya City Eliud Ambokile, ambaye kwa sasa anaongoza kwa kupachika mabao, akiwaacha washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kwa sasa anapata taabu sana kutokana na kusumbuliwa na ukame wa mabao.
Ambokile mwenye mabao 8 ni mzawa, amewapiku washambuliaji wa kimataifa Okwi na Kagere wenye mabao 7, amesema kuwa akiwa ndani ya uwanja kwenye mechi mbili alizocheza ile ya KMC na JKT mabeki wanamkamia.
"Ligi haitabiriki kwa sasa hivyo kuna ugumu wa kufanikiwa kufunga, mabeki wananikamia sana maana wengi nimekuwa nikiwasumbua uwanjani, ila sasa nadhani wanapewa maelekezo maalumu na walimu ili wahakikishe hawanipi nafasi ila hilo halinipi wasiwasi kwa kuwa bado tuna mechi nyingi.
"Kila siku najitahidi kuweza kufanya vizuri na tunashirikiana kwa ukaribu na wachezaji wenzangu ili kuweza kupata matokeo, wakati mwingine ratiba inakuwa ni ngumu kwetu," alisema.
Mchezo wa mwisho kufunga ilikuwa dhidi ya Mwadui ambao walitoka sare ya kufungana mabao 2-2.
Kutoka Championi
0 COMMENTS:
Post a Comment