November 17, 2018


 
Timu ya Taifa ya Uganda, leo imefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) itakayofanyika mwakani nchini Cameroon baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cape Verde.

Kikosi hicho ambacho Juuko Murshid anayechezea timu ya Simba kimefanikiwa kupenya baada ya kufikisha pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ya kundi L ambalo Tanzania ipo pia.

Mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Mandela nchini Kenya ulianza kwa kasi ambapo kila timu ilipambana kupata matokeo na dakika 45 za kipindi cha kwanza ziliisha bila kufungana.


Dakika ya 78 mchezaji wa Kenya, Patrick Henry alifunga bao la ushindi kwa kumalizia pasi iliyopigwa na Walusimbi Godfrey akafunga kwa  kichwa kilichomshinda mlinda mlango wa Capeverde.


Juuko alifanikiwa kuisaidia timu yake katika hatari nyingi kwa kuwa aliweza kuokoa hatari zaidi ya mara tatu hali iliyopelekea kuweza kupewa kadi ya njano akiwa uwanjani, Emmanueli Okwi hakucheza kutokana na kuwa na kadi.


Kwa matokeo hayo Tanzaina inapaswa kushinda kesho katika mchezo wake dhidi ya Lesotho ili kufikisha pointi nane kabla ya mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda nyumbani.

9 COMMENTS:

  1. Naomba mwandishi awe makini na uandishi wake,Timu iliyocheza ni ya Uganda na mfungaji wa goli ni wa Uganda sio Kenya.

    ReplyDelete
  2. Na uwanja wa Mandela upo Uganda sio Kenya. Timu zilicheza Uganda Bwana!

    ReplyDelete
  3. Mmendika utumbo tu!

    Sasa ndo nini uwanja upo kenya na mfungaji yupo kenya halafu inafuzu uganda,okwi naye yupo!Utumbo tu

    ReplyDelete
  4. Mmendika utumbo tu!

    Sasa ndo nini uwanja upo kenya na mfungaji yupo kenya halafu inafuzu uganda,okwi naye yupo!Utumbo tu

    ReplyDelete
  5. hivi salehe jembe mwenyewe upo au ulikufa!!! maana hii blog ilikuwa the best ulipokwepo ndio maana naauliza hivi kweli upo? na kama upo matakataka haya unayaona? nawe umeridhika kabisa. kama upo toka hadharani uombe radhi la funga blog yako.jitafakari kama vipi ondoa kabisa hii blogu nimewasilisha

    ReplyDelete
  6. waandishi wa zamani walitakiwa wawe wamefaulu masomo ya jiografia na historia ila kwa sababu ya vyuo feki vinazalisha waandishi feki haya ndio matokeo yake

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic