November 17, 2018


Winga wa timu ya taifa, Taifa Stars anayeichezea klabu ya Difaa El Jadida ya nchini Morocco Simon Msuva amesema kuwa kikosi chao kipo fiti kuwavaa wapinzani wao Lesotho kesho.

Stars ipo kundi L itawavaa wapinzani wao bila nahodha Mbwana Samatta anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji kutokana na kuwa na kadi mbili za njano.

"Siyo mechi nyepesi kwetu licha ya kukosekana Samatta ambaye alikuwa anahitajika kikosini, tumejianda kupata matokeo, tunatambua umuhimu wa mechi na tukishinda tutakuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu Afcon," alisema.

Meneja wa Stars, Dany Msangi alisema kuwa wachezaji wana morali ya kufanya vizuri kwa kuwa kikosi kiliwasili jana Lesotho baada ya kambi nzuri ya siku 10, ila Shomari Kapombe na Rashid Mandawa kwa bado wanaumwa," alisema.

1 COMMENTS:

  1. Duuuh Mbona Sasa Kama Mandawa Ndo Alikuwa Awe Mrithi Mzur wa Samata!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic