Uongozi wa Singida United, umefunguka kuwa upo kwenye mchakato wa kuwachukua nyota wawili ndani ya Simba watakaoachwa kwa mkopo katika usajili wa dirisha dogo.
Singida United msimu huu hajianza vizuri kutokana na kuondokewa na baadhi ya wachezaji wake ikiwa ni pamoja na Peter Manyika ambaye ametimkia Kenya kwa kushindwa kulipa stahiki zake.
Mkurugezi wa Singida United, Festo Sanga amesema kuwa wana mpango wa kuimarisha kikosi chao msimu huu kwenye dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15 ili kuweza kuongeza makali yao.
"Tupo kwenye mazungumzo ya mwisho kuwapata wachezaji wawili kutoka Simba ambao wataachwa kwa mkopo katika dirisha dogo ili tuimarishe kikosi chetu ambacho kimekuwa chepesi sana tunahitaji mshambuliaji na kiungo," alisema.
Singida United wamecheza michezo 14 wamepoteza 6, wameshinda 5 na kutoa sare 3 wanashika nafasi ya 9 baada ya kukusanya pointi 18.








hao Singida c walitoa sadaka feisal na beki juu, leo hii chaliiii, wanamix mahaba kwny mpira, ikowapi TOTO la Yanga ya Mwanza?
ReplyDeleteIko wapi jukuu la simba Nyota Nyekundu ya mtaa wa Kongo?
DeleteYanga waliwalipa JKU gharama za feisal Kwan alikuwa na mkataba kule wakat singida walipita juu. Elisha Muroiwa Yanga walimkataa. Singida wamepoteza muelekeo kwa ukosefu wa fedha
Deletehamna kuwapa wachezaji wao si waligawa wachezaji kwa yanga bora hii timu ishuke daraja
ReplyDelete