November 15, 2018


Meneja wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa kuchukua nafasi ya Slavisa Jokanovic kuwa kocha wa Fulham ingawa tayari Claudio Ranieri alikuwa amepewa. (Daily Mirror)

Huku meneja wa zamani wa Chelsea na Tottenham, Andre Villas-Boas pamoja na kocha wa zamani wa Monaco Leonardo Jardim wote wameikataa nafasi ya kuiongoza Fulham. (Telegraph)

Meneja mpya wa Fulham Ranieri, anataka kumsajili mlinzi wa Liverpool Joel Matip, 27 mwezi Januari. (A Spor, via Talksport)

Real Madrid iko tayari kumchukua mmoja wa washambuliaji wa Paris St-Germain kama klabu ya Ufaransa itawauza wachezaji wake kutokana na sababu za matumizi zaidi ya kifedha. Wachezaji hao ni Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19. (AS - in Spanish)

'Mechi za kirafiki' ziliisaidia City - Mourinho
Fifa inavichunguza vilabu vitano vya ligi ya England kuhusu uvunjwaji wa kanuni za usajili wa wachezaji wa kigeni ambao wako chini ya umri wa miaka 18.

Timu hizo zitafugiwa kufanya usajili ikiwa zitakutwa na hatia ya kukiukwa na kanuni za usajili. (Daily Telegraph)

Kipa wa Manchester United David de Gea, 28, anaendelea na majadiliano kuhusu kusaini mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa de Gea utaisha muda wake katika kipindi cha kiangazi lakini klabu inataka kumuongezea miezi 12. (London Evening Standard)

Everton inataka kumsajili mlinzi wa kati Chris Smalling, 28,mwishoni mwa msimu huu wakati ambao mkataba wake utakuwa umeisha. (The Sun)

Kiungo wa kati wa Manchester City na England Phil Foden,18 anakaribia kusaini mkataba mpya wa miaka sita. (Daily Telegraph)

Meneja wa England Gareth Southgate atamtumia kwa mara ya kwanza goli kipa wa Southampton Alex McCarthy, mlinzi wa Brighton Lewis Dunk na mshambuliaji wa Bournemouth Callum Wilson katika mechi ya kirafiki dhidi ya Marekani itakayofanyika siku ya alhamisi. (Daily Mirror)

Chelsea wanavutiwa kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, 20, katika msimu wa kiangazi. (The Guardian)

Chelsea wako tayari kusikiliza ofa ya mkopo ya mlinzi wa kati na nahodha Gary Cahill, 32, ambaye mkataba wake unaisha mwisho wa msimu. (Daily Mail)

Roma inajiandaa kumsajili mchezaji wa Manchester United Ashley Young, 33 mwezi Januari. (The Sun)

Wolves inatamani kumsajili mlinzi wa Argentina Marcos Rojo, 28, ambaye atakuwa huru kuondoka Manchester United mwezi Januari. (Birmingham Mail)

Newcastle inavutiwa na Miguel Almiron mwenye umri wa miaka 24 ambaye ni kiungo wa kati wa Paraguay anayecheza ligi ya nchini Marekani. (The Chronicle)

Kwa mujibu wa BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic