November 14, 2018


Timu ya Tanzania ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 23 leo imekubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya timu ya Burudi katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu kushiriki michezo ya Afcon.

Timu ya hiyo ipo chini ya kocha Bakari Shime imepoteza mchezo huo baada ya kuonyesha juhudi kipindi cha kwanza ambapo waliweza kwenda sare ya kutofungana ila kipindi cha pili mambo yakabadilika.

  Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Prince Louis Rwagasore, Bunjumbura umemalizika  kwa Tanzania kushindwa kuchukua pointi tatu.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 59 kwa njia ya Penati lilifungwa na Shaban Mabano na bao la pili lilifungwa dakika ya 79 na Cedric Mavugo.

Mchezo wa marudio utachezwa Tanzania ambapo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu, timu ya Taifa itatakiwa ishinde kwa zaidi ya mabao 3.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic