November 14, 2018


Kikosi cha timu ya Simba kilicho chini ya Kocha Mkuu Patrick Aussems kimeanza kuwavutia kasi wapinzani wao Mbabane Swallows kutoka Swaziland kwa kucheza na mabingwa kutoka Malawi ili kuweza kujiweka sawa.

Mbabane ni mabingwa katika ligi ya Swaziland watamenyana na Simba katika mchezo wa ligi ya Mabingwa ya Afrika unaotarajiwa kuchezwa Novemba 27 au 28 Dar es Salaam na marudio kuwa Desemba 3 au 4 nchini Swaziland.

Ofisa habari wa Simb, Haji Manara amesema kuwa wamejipanga kisai cha kutosha kuweza kufanya vizuri michuano hiyo kwa kuwa wanajua mashabiki na taifa linahitaji ushindi.

"Kikosi chetu kipo imara na tutaanza kufanya majaribio na mabingwa kutoka Malawi, Big Bullets FC ni timu nzuri na kipimo kwetu kuelekea katika michuano ya kimataifa, mashabiki watupe sapoti katika kila hatua," alisema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic