DStv yatangaza neema kwa wateja wake msimu huu wa sikukuu!
Katika msimu huu wa sikukuu ambapo watu wengi hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, MultiChoice Tanzania imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake na wale wanaojiunga na huduma za DStv kupitia kampeni yake maalum ijulikanayo kama ‘Ni Muda wa Kukiwasha na DStv’.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema wateja wa DStv sasa watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia Soka, Filamu, Tamthilia, Katuni na vipindi mbali mbali vya watoto vitakavyoileta familia pamoja na kuimarisha upendo.
Amesema DStv imekuwa mara kwa mara ikiwatunuku wateja wake waliopo na wapya zawadi na ofa kabambe huku wakiendelea kupata burudani ya uhakika muda wote. “Mwaka huu kama kawaida umekuwa mwaka wa neema kwa wateja kwani tumekuwa na mfululizo wa zawadi kwa wateja wetu”
Kwa wateja wapya wanaojiunga na DStv msimu huu watapata ofa maalum ya kuunganishwa kwa shilingi 79,000 pamoja na zawadi maalum ya kifurushi cha mwezi cha Bomba bila malipo ya ziada. Ofa hii itaendelea kwa muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 15 Novemba 2018 na ni kwa nchi nzima.
Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum, amesema kuwa ofa hii ni zawadi ya kufunga mwaka kwa wateja wapya wa DStv kwani katika kipindi cha miezi miwili wataweza kuunganishwa na DStv kwa gharama ya shilingi 79,000 tu na zaidi ya hapo kupewa kifurushi cha Bomba cha mwezi mmoja bila malipo ya ziada.
“Mbali na kuongezwa kwa chaneli na maudhui kedekede kwa wateja walipo wa DStv, pia kwa wale ambao bado hawajajiunga hatujawasahau, sasa tunawapa ofa hiii kabambe ya kujiunga kwa gharama nafuu na zaidi ya hapo wapate kifurushi cha mwezi mmoja bila malipo. Hii ni zawadi yetu ya sikukuu kwa wateja wetu” alisema Salum Salum.
Amesisitiza kuwa ofa hii ni kwa nchi nzima na tayari wameshajipanga na mawakala wote kuhakikisha kuwa ofa hii inapatikana nchi nzima. “Mtu yeyote asiwe na wasiwasi wa jinsi ya kuunganishwa kwa ofa hii. Tunao mawakala wetu wa usambazaji na ufundi nchi nzima, hivyo hata walio maeneo ya vijijini huduma hii watapata.
0 COMMENTS:
Post a Comment