Bwire amesema kuwa wana kila sababu za kufanya vizuri kwa kuwa mchezo wao wa mwisho walichukua pointi tatu mbele ya Stand United, mchezo uliochezwa uwanja wa Mabatini.
"Timu ipo sawa na tumejiandaa kiasi cha kutosha kuweza kuwapapasa wanaofuata ambao kwa sasa ni Azam FC, tupo tayari," alisema.
Azam FC ni vinara kwenye ligi, hawajapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kutoa sare 3 na kushinda michezo 9 kati ya 12 waliyocheza wakiwa na pointi 30.
0 COMMENTS:
Post a Comment