Mkutano huu ulifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere mjini Dar es Salaam ambapo Swedi Nkwabi alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ukurugenzi ya Simba
Swedi alikuwa mgombea pekee baada ya Mtemi Ramadhani kujitoa dakika za mwishoni na amepita bila kupingwa kwa kupata kura 1,579 za Ndiyo kati ya kura 1,628 zilizopigwa.
Katika nafasi za Ujumbe, viongozi wote waliomaliza muda wao, Iddi Kajuna, Said Tuliy, Ally Suru na Jasmine Costa wameangushwa.
Waliochaguliwa katika nafasi za Ujumbe ni Hussein Kitta Mlinga, Dk. Zawadi Ally Kadunda, Suleiman Haroub Said, Mwina Mohammed Kaduguda na Asha Ramadhani Baraka.








0 COMMENTS:
Post a Comment