November 27, 2018


Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera,  amesema hana mpango wa kusajili wachezaji wapya wakati wa dirisha dogo la usajili kwa sababu kuna wachezaji zaidi ya kumi kwenye timu hiyo walio na matatizo na klabu kuhusu maslahi yao, wakimlilia kila mara na bado hayajatatuliwa.

Zahera ameyasema hayo baada ya  Yanga kimewasili Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo ikitokea Bukoba mkoani Kagera ambako ilicheza na timu ya Kagera Sugar na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kupaa hadi nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikifikisha alama 32 nyuma ya Azam huku ikibakiwa na mchezo mmoja.

“Huwezi kukaribisha mtoto wa mjomba wako ukaja kuishi naye kwako wakati wewe mwenyewe una matatizo chungu nzima na watoto wako wanakosa hata pesa ya ada ya shule au chakula, siwezi kusajili wachezaji wengine wakati hawa waliopo bado kuna matatizo ambayo hayajatatuliwa,” alisema na kuongeza kwamba lengo lake siyo kubeba kombe wala ubingwa kwa sababu kikosi chake bado kina changamoto nyingi.

Yanga ambayo kabla ya kucheza na Kagera ilicheza na Mwadui FC ya Shinyanga na kuilaza kwa mabao 2-1, itakabili JKT Ruvu katika mechi ijayo.

1 COMMENTS:

  1. Laiti kama ungelikua unaongea kweli haki ya mungu ungelikwenda peponi,timu ina matatizo lukuki na hakuna hata moja lenye dalili za utatuzi then mnataka kusajili wachezaji wengine,mpaka leo yondani na kakolanya hakijaeleweka,acheni kujiamini kwa matokeo yakubahatisha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic