WAKILI MSOMI TFF AFUNGIWA KUJIHUSISHA NA SOKA
Na George Mganga
Kamati ya maadili ya ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Mwenyekiti wake, Hamidu Mbwezeleni imetangaza kumfungia maisha kutojihusisha na masuala ya soka aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocutus Kuuli.
Kuuli amefungiwa kufuatia sakata la uchaguzi Simba ambapo alihojiwa kwanini ameamua kuuzuia mchakato wake kipindi unaanza na kupewa siku tatu kwa ajili ya kutoa majibu.
Wakili hiyo alipewa siku hizo na Katibu Mkuu wa Shirikisho, Wilfred Kidao lakini hakuweza kujibu chochote na kisha baadaye kuja na majibu ya dhihaka na lugha kali kwa Kidao.
Hata hivyo, Kuuli baadaye kabla hajafungiwa ilielezwa kuwa angetangaza kuachia nafasi hiyo ndani ya TFF akielezwa kukerwa kuingiliwa kwenye majukumu yake ya kazi.
Licha ya kuuzia mchakato wa uchaguzi Simba, klabu hiyo iliendelea nao kama kawaida ambapo jana rasmi imefanikisha kufanya uchaguzi wake na kuwapata viongozi wapya.
AMEKUWA BURUDOZA AMESHACHONGA BARABARA YA KARIA SASA AMETUPIWA VIRAGO,NDIO MJIFUNZE KUWA HAKUNA RAFIKI WA KUDUMU DUNIANI ZAIDI YA SALA YAKO TUU
ReplyDelete