November 2, 2018


Kabla hata ya dirisha la dogo kuelekea kufunguliwa na ligi ikiwa bado imepamba moto, unaambiwa Kocha Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems amepania kuwatema wachezaji kadhaa katika kikosi chake.

Taarifa za udukuzi zinaeleza kuwa Aussems ana mpango wa kuwapeleka baadhi yao katika timu zingine kwa mkopo huku baadhi akiwaacha kabisa.

Aidha, Mbelgiji huyo yuko kwenye mipango ya kuwataka mabosi wake kuleta vifaa vingine ambayo vitakuwa na nguvu ya kuendana na kasi anayoitaka na kuisaidia Simba kwenye mechi za kimataifa.

Inaelezwa kuwa Aussems ana mpango wa kumrejea Mohammed Rashid katika timu ya Tanzania Prisons alipotokea kwa mkopo baada ya kuona hana mchango mkubwa kwa sasa.

Aidha, Aussems ametaka kuiboresha safu ya kiungo kwa kutaka aletewe mchezaji mwenye utulivu ambaye ataweza kuwa mnyumbulifu wa kupika mipira na kuwalisha washambuliaji.

Inaelezwa pia Mbelgiji huyo hawahitaji wachezaji Mghana, Nicholous Gyan na Mnyarwanda Haruna Niyonzima ambao wamekuwa si sehemu ya kikosi cha kwanza.

Yusuph Mlipili ni jina mojawapo pia ambalo linatajwa kupelekwa kwa mkopo mahala pengine.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic