YANGA YAPATA 'BACK UP' HII YA MAANA KUELEKEA MECHI NA NDANDA
Uongozi wa klabu ya Yanga umewataja wachezaji Ibrahim Ajibu na Papy Tshishimbi kuanza mazoezi jana na wenzao kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mratibu wa timu, Hafidh Saleh, ameeleza kuwa Ajibu na Tshishimbi wameanza mazoezi hayo tayari kuelekea mchezo ujao dhidi ya Ndanda FC.
Wachezaji hao walikuwa majeruhi jambo ambali lilipelekea kukosa mchezo uliopita dhidi ya Lipuli ya Iringa ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Yanga itakuwa na kibarua hicho kizito kitakachopigwa wikiendi hii na Ndanda ambao waliilazimisha Simba kwao Mtwara kwenda suluhu ya kutokufungana.








0 COMMENTS:
Post a Comment