November 8, 2018


Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea kufunguliwa kwa dirisha la usajili katika Ligi Kuu Bara, uongozi wa timu ya Azam FC upo katika hatua za mwisho za mazungumzo na mchezaji wa zamani wa Yanga Obrey Chirwa ambaye aliondoka na kwenda Misri kuchezea timu ya Isimailia, huenda akasijiliwa na Azam dirisha dogo.

Imeelezwa kuwa Chirwa amevunja mkataba wake na timu hiyo baada ya kutokulipwa stahiki zake na taarifa za kuaminika zikadai kwamba amerejea ili kujiunga na Yanga ila baada ya kocha Mkuu wa, Yanga Mwinyi Zahera kumgomea ndipo Kocha wa Azam, Hans Pluijm akapendekeza asajiliwe.

“Kocha Pluijm amemtaka awe ndani ya timu kutokana na uwezo, wake hivyo kama atapitishwa anaweza kutangazwa muda wowote kuanzia sasa, pia ni rafiki mkubwa wa Donald Ngoma ambaye naye ni raia wa Zambia hivyo kuna jambo linaendelea,”  kilieleza chanzo.

Meneja wa Azam, Philip Alando, alisema kuwa uongozi utatoa taarifa kuhusu masuala ya usajili muda ukifika kwa kuwa timu ina mipango mingi hasa katika kuimarisha kikosi.

Hapo awali ilielezwa kuwa klabu yake ya zamani, Yanga ilikuwa kwenye harakati za kumrejesha lakini Azam wamefanikiwa kuwapiga kete mabingwa hao wa kihistoria.

5 COMMENTS:

  1. Acheni uchonganishi nani amewaambia Yanga wanamtaka huku nyuma Kocha wa Yanga alishasema hana mpango wa kumsajili Chirwa kutokana na nidhamu mbovu sasa nyie salehjembe blog mnasema eti Azam wameipiga bao Yanga ebu acheni udaku na mwandike kwa kufuata miiko ya uandishi bila kuweka umbea na ushabiki

    ReplyDelete
  2. Umakini ni jambo la msingi sana, hivi Donald Ngoma ni raia wa Zambia kweli? Mie najua yule ni mzimbabwe.

    ReplyDelete
  3. donald ngoma raia wa zambia!! acha upuuzi

    ReplyDelete
  4. Mwandishi hujielewi na hauko makini kabisa,facts ni
    1.Ngoma sio raia wa Zambia ni Zimbabwe
    2.Yanga hawajafanyiwa umafia wowote kocha alisha weka wazi hamtaki Chirwa ndipo Azam wameamua kumchukua,umafia uko wapi hapo?

    ReplyDelete
  5. Hivi mjomba walau elimu ya msingi ulihitimu kweli? Unatia Shaka kuhusu uelewa wako wa Mambo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic