November 8, 2018


Baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Stand United mchezo uliochezwa Uwanja wa Mabatini Pwani, Ofisa habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amefunguka siri ya ushindi huo.

Bwire amesema kuwa timu yao haina tatizo lolote kuhusu matokeo yao yaliyopita bali wanajifunza kupitia makosa na kufanya kazi zaidi ili kuendelea kupata ushindi zaidi.

“Mpira una matokeo ya tofauti ila kwetu sisi tunaamini kwamba tuna uwezo wa kupambana na kupata matokeo kwa timu yoyote, masuala ya kushindwa kwetu hayapo ilitokea mwanzo kwa kuwa haikuwa ni mpango wa Mungu sasa kazi ndo imeanza,” alisema.

Ruvu Shooting waliweka rekodi kwa kufungwa jumla ya mabo 9 katika mechi mbili ,ushindi huo unawafanya wafikishe pointi 16 baada ya kucheza michezo13 na kushjika nafasi ya 12.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic