November 8, 2018


Uongozi wa timu ya Alliance FC, umechekelea kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliochezwa uwanja Nyamagana, Mwanza.

Ofisa habari wa Alliance, Jacson Mwafulango alisema  wameonyesha uwezo mkubwa katika mchezo wao hali ambayo inawafanya waendeleze kusambaza upendo kwa mashabiki wake.

“Mtibwa Sugar walikosea kitu kimoja kwa kucheza mpira wa chini na pasi nyingi hicho ndicho kimewagharimu kwa kuwa mchezo huo sisi tumeuzoea na tukawazidi maarifa.

“Tumeshinda mchezo wetu kwa ushindi mdogo wa bao moja ila kitu cha muhimu ni pointi tatu, uwanja wetu wa nyumbani ni lazima tuutumie vizuri,” alisema.

Matokeo hayo yanawafanya Alliance kuwa nafasi ya 16 baada ya kucheza michezo 16 na kufikisha jumla ya pointi 13, Mtibwa Sugar wakiendelea kubaki nafasi ya nne wakiwa na pointi 23 wamecheza michezo 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic