November 18, 2018


Imeelezwa kuwa mabosi wa klabu ya Yanga wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa mchezaji, straika Nelson Senkatuka kutoka Bright Star ya Uganda.

Straika huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda The Cranes, ameingia kwenye rada za Yanga kabla ya dirisha dogo la usajili kufunguliwa.

Taarifa imeeleza Senkatuka atawasili hapa nchini jijini Dar es Salaam kuja kumalizana na mabosi wa Yanga siku yoyote kuanzia leo.


Nyota huyo ambaye inaelezwa ana miaka 21 akiwa amezaliwa mwaka 1997 anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Donald Ngoma ambaye aliondoka na kuelekea Azam.

Awali ujio wa Mkongo, Heritier Makambo ulichukuliwa kama mbadala wa Ngoma lakini kwa mwenendo wake ulivyo bado hajaonesha ukomavu wa kutosha ambapo Yanga imewalazimu wasake mbadala mwingine kujaza nafasi hiyo.




1 COMMENTS:

  1. Mbadala Tena kivipi wakati mlisema makambo ndio kila kitu Tanzania

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic