November 15, 2018


Wakati kikosi cha Yanga kikiwa kimeandamwa na majeruhi kadhaa mpaka sasa, Uongozi wa Yanga umemrejesha Mkongo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi ndani ya kikosi hicho juzi Jumanne na kuanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.

Kiungo huyo alikuwa nje kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo yalisababisha kukosa mechi zaidi ya tatu msimu huu kutokana na kutokuwa imara kiafya.

Mratibu wa Yanga, Hafidhi Salehe alisema kuwa mchezaji huyo ataendelea kufanya mazoezi ila mchezo wao na Reha uliopigwa jana Jumatano hakuwa sehemu ya wachezaji waliocheza kwa kuwa ndiyo kwanza ameanza mazoezi.

“Kurejea kwake ni jambo jema na la kheri kwa timu sababu anakuwa ameongeza nguvu hivyo hakuna tatizo mchezaji ambaye amesalia kwa sasa yupo nje ni Juma Mahadhi pekee,” alisema Hafidhi ambaye ni miongoni mwa watu waliodumu kwenye ofisi za Yanga zaidi ya miaka 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic