November 2, 2018



Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Mwinyi Zahera amesema kuwa hana hofu na mechi ambazo atacheza nje ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kuwa anatambua vizuri viwanja vya Tanzania.

Yanga wamecheza michezo 9 kwnye ligi kuu ambayo yote wametumia uwanja wa Taifa na kuwafanya wafanikiwe kushinda michezo 8 wakiwa wamepata sare mchezo mmoja huku wakiwa nafasi ya pili baada ya kujikusanyia pointi 23.

"Nimefanikiwa kuvitambua viwanja vingi vya Tanzania hasa katika ubora hakuna viwanja vizuri vingi ni vibaya, timu yetu inafanya mazoezi katika uwanja mbaya hivyo tayari wachezaji wanamudu mazingira yote.


"Nafurahia kuwa nje kwa kuwa ukiwa mgeni unakuwa hauna presha kubwa kuliko ilivyokuwa kwa sasa, napenda na tupo tayari kupambana kuhakikisha tunafanya vizuri ," alisema.


 Mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Ndanda FC kutoka Mtwara wakiwa na rekodi ya kukusanya pointi 25 katika uwanja wa taifa.
 

6 COMMENTS:

  1. Acha kuimba ndombolo hapa...katika uwanja wako nzuri wa Dar unaishia kupata ushindi wa goli moja...ni mechi ya alliance tu ndio mliwazidi bao tatu..kawaida we we ni kagoli kamoja au mawili..na ball possession unazidiwa..huko mikoani we we utatoa safe au kufungwa tu!kila LA hero mzee wa ndombolo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli we sio mtu wa mpira ni mechi mbili tu ambazo yanga wamepata ushindi wa goli moja moja lakin simba wao wamesahau kuna mechi mbili wao hawajapata goli hata moja mechi na ndanda na mechi na mbao

      Delete
  2. Saleh jembe acha kuzingua kuna ukiboko hapo?

    ReplyDelete
  3. Has walishaanza lalamika viwanja vibovu hata hawajatoka nje ya Dar!

    ReplyDelete
  4. Washabiki tunaendelea kuwa washabiki. Siwez ingilia nn kocha anafanya. Kocha anajua...sisi Simba wakat mwingine tunajiamin kupitiliza hatuziheshimu timu ndoho. Mechi na ndanda kila mtu Ali tunaweza kushinda lakn had mwisho majanga. Mech na mbao tuliwazid tukaja tukakosa utulivu na hata ya yanga pia. Kwahyo shda ni cc wenyewe na wala so ubora wa mbao wala ndanda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic