December 26, 2018



NAHODHA wa timu ya Simba, John Bocco amesema kuwa kinachomfanya ashindwe kufunga mabao ni kutokana na kukamiwa na mabeki akiwa uwanjani hali inayomfanya ashindwe kung'ara.

Bocco amekuwa katika wakati mgumu wa kufunga mabao kwenye Ligi Kuu pamoja na mashindano ya kimataifa kwani mpaka sasa ligi Kuu ana mabao 2 Simba wakiwa wamecheza michezo 13 na kimataifa ana mabao 2, Simba wakiwa wamecheza mechi 4.

Bocco amesema kuwa kikubwa ambacho wanakiangalia ni ushindi hivyo hana maumivu anaposhindwa kufunga kwa kuwa ni sehemu ya mchezo.

"Tunapambana kutafuta matokeo tukiwa uwanjani, hali ya kushindwa kufunga inatokea kutokana na ushindani uliopo ila ni jambo la kawaida kutokea kwa mchezaji yoyote akiwa uwanjani.

"Kila timu hesabu zake ni kushinda hivyo malengo yanapotimia kinachofuata ni kutatua makosa ambayo tumeyafanya na kusonga mbele kiushindani," alisema Bocco.

1 COMMENTS:

  1. Huyo Boko jinsi anavyokosa magoli tema mate chini kama karogwa vile. Yeye kama anaamini sababu ya kukosa mabao ni kukamiwa na mabeki mimi basi nitampa dawa ya kutibu ugonjwa huo kwa sharti la lazima afuate maelekezo nitakayo mpa, mimi by professional ni mtaalam wa fitnes. BOKO anakosa kujiamini anapoingia kwenye kumi na nane kitu kinachomsababishia kuwa na papara inayosababishwa na uoga na kumpelekea kuchukua maamuzi ya hovyo. BOKO ni fowadi namba mmoja wa Simba kimajukumu na ni kapteni anatakiwa kuwa anawaongoza wenzake kujifunza kutoka kwake na sio kumuelekeza cha kufanya. Anatakiwa kuwa na mwili uliotimia,miguu iliyotimia lakini kikubwa zaidi anatakiwa kuwa na kichwa kilichokamilika kufanya maamuzi sahihi na kamwe maamuzi sahihi hayawezi kuchukuliwa katika hali ya papara. Sasa nini cha kufanya John Boko kurejesha hali ya kujiamini. 1(1) Anatakiwa kufanya mazoezi ya kimkakati kuongeza uimara wa mwili wake. 2(2) Anatakiwa kuwa na muda wa kutosha wa kupumzika ikiwemo kulala kwa nafasi baada ya mazoezi. 3(2)Anatakiwa kuondosha mawazo ya lazima afunge yeye anapokuwa ndani ya kumi na nane au anapopata pasi ya mwisho na badala yake anatakiwa kurilax akiwa ameumiliki mpira huku akiwa na option tatu za haraka kabla ya kufanya maamuzi ya mwisho (1) kufunga(2) kuangaza kama kuna mchezaji mwenzake aliekuwa kwenye nafasi bora zaidi ya kufunga zaidi yake(3) kusababisha penalt. Hakuna haja fowadi alie kwenye kumi na nane kuwa na wahaka anapokuwa ameumiliki mpira na ndio maana wachezaji wanaojitambua inakuwa rahisi kufunga kwani kitendo cha fowadi kuingia kwenye kumi na nane ya adui beki tayari imeshasalimu amri kilichobakia ni kutizama kudra za Mungu na uwezo wa fowadi kwani makeke yeyote ya beki kwa fowadi pinzani ndani ya boksi madhara yake ni makubwa beki lazima awe mpole . Kwa hivyo cha kufanya Boko ni kuwa mtulivu na mwenye kujiamini na kuwa kinganganizi wa kumiliki mpira yaani iwe kupokonywa mpira katika eneo la hatari iwe vita isiwe jambo rahisi akiweza kufanya hayo basi hatua ya makundi Caf itamkumbuka daima, yupo vizuri ila ayafanyie kazi haya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic