December 1, 2018


Straika mwenye balaa la aina yake katika kikosi cha Simba, Meddie Kagere, amesema wanachohitaji kwa sasa ni kufanya vema kwenye mchezo dhidi ya Mbabane Swallows ili kusonga mbele hatua inayofuata.

Simba itakutana na Mbabane Disemba 4 huko Swaziland ukiwa ni mchezo wa marudiano ikiwa ni baada ya kuwafunga hapa Dar es Salaam kwa mabao 4-1.

Kagere ambaye alifunga bao 1 kwenye mechi hiyo likiwa ni la tatu kwenye mchezo, ameeleza kuwa wanahitaji kushinda na akikiri kuwa wapinzani wao ni wazuri.

“Tunahitaji kufanya vyema katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane ili tuweze kusonga mbele. Lengo letu ni kuona tunafanikiwa kusonga mbele katika michuano hii kwa kuwafunga wapinzani wetu katika mchezo wa marudiano.

“Mbabane ni timu nzuri hivyo itajiandaa kuona inafanikiwa kufanya vizuri, lakini naamini mwalimu atafanyia kazi makosa yaliyojitokeza ili kufanya vizuri katika mchezo huo.” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic