December 1, 2018


Msafara wa watu zaidi ya 30 wakiwemo wachezaji 21, kesho Alfajiri unatarajiwa kuondoka kwenda Eswatini, huku John Bocco na Meddie Kagere wakitamba lazima washinde.

Mbabane Swallows itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Mavuso Sport Center. Katika mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar, Simba ilishinda mabao 4-1.

Hata hivyo, kabla ya Simba kuondoka kesho, tayari Simba ilimtuma mratibu wake, Abassi Ally kwenda kuweka mazingira sawa kabla ya timu kuwasili hiyo kesho Jumapili.

Mkuu wa Kitego cha Mawasiliano cha Simba, Haji Manara alisema, msafara huo utaondoka na Shirika la Ndege la Ethiopia na wanatarajiwa kufika siku hiyohiyo.

4 COMMENTS:

  1. kila lenye kheri wawakilishi wa nchi TZA

    ReplyDelete
  2. Nawaombea chama langu, kwani binafsi nawaamini.

    ReplyDelete
  3. Najua mtafanya kweli maana mmedhamiria kufanya kweli mwaka huu.

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  4. All the best wataniii... Najiskia vizuri sana kuwakilishwa nanyi msimu huu. Kwakweli kikosi chenu ni motoooo.... Ila VPL ushabiki mbele😁

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic