December 21, 2018



Kamati ya saa 72 imewafungia wachezaji  wawili  huku wengine wakipelekwa katika kamati ya nidhamu na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)

 Wachezaji ambao wamefungiwa ni pamoja na Hassan Dilunga wa Simba na Ibrahim Job wa Lipuli  huku mchezaji wa Yanga Andrew Vicent ‘Dante’ na wengine ambao  majina yao hajabainishwa  wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu.

 Dilunga na Job wamefungiwa kutokana na wachezaji hao kuchelewa kutoka uwanjani wakati timu zikienda kwenye mapumziko kitendo ambacho sio sahihi wakati wenzao wakiwa vyumbani.

Kaimu Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Ibrahim Mwayela amesema kuwa wachezaji wamesimamishwa kwa mechi tatu na wengine wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu.

“Dilunga na Job wamefungiwa mechi tatu na tayari wameanza kutumikia adhabu zao sababu klabu zilishaarifiwa na watalipa faini ya kiasi cha shilingi laki tano kila mmoja.

 “Wachezaji kama Vicent Andrew wa Yanga pamoja na viongozi wengine wamepelekwa  katika kamati ya nidhamu na hadhi za wachezaji kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu," alisema.


6 COMMENTS:

  1. Adhabu nyingine hazina uwiano na kosa lililotendeka. Kuchelewa kutoka uwanjani kwa wachezaji wanaojisahau wakisalimiana ndio wafungiwe kucheza mechi 3?na fatni laki 5? Busara ipo wapi?

    ReplyDelete
  2. Tff wamegeza faini nimladi ndio soka letu

    ReplyDelete
  3. Lakini hii imekaaje jamani? TFF kweli wanaamini na kuyatilia maanani mambo ya kishirikina? Kwa sababu ukweli halisi wa adhabu waliopewa akina Dilunga sio kuchelewa kutoka uwanjani bali ni ile sababu iliyowafanya wawili hao kutegeana kutoka uwanjani ambayo inasemakana ni ushirikina. Hii TFF ina viongozi wa hovyo kiasi cha kushangaza. Kumfungia mchezaji mechi tatu kama vile kampiga mchezaji mwenzake kichwa cha makusudi kumbe vile kachelewa kutoka uwanjani ni jambo linalotia aibu kiasi cha kukosa maelezo ila wahusika wajue wanakoelekea kunatia shaka kubwa katika kuleta maendeleo ya soka nchini kwa sababu vile vitu vya maana havitiliwi maanani vinavyotiliwa maanani pale TFF ni yale mambo ya kijinga.

    ReplyDelete
  4. hawa tiefuefu ni wapumbavu,wanaacha kuwafungia kina makambo,ngassa na dante waliofanya vurugu na kupiga watu uwanjani wanafungia waliochelewa kutoka uwanjani ......shenztypu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic