December 21, 2018


Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana FC utakuwa ni mgumu ila kipaumbele kwa timu ni kupata ushindi.

Simba watacheza na Nkana FC katika uwanja wa Taifa jumapili wakitakiwa kushinda bao 1-0 baada ya kukubali kufungwa bao 2-1 katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Zambia.

"Tulikubali kupoteza mchezo wa kwanza ugenini baada ya kushindwa kupata matokeo mazuri, wapinzani wetu walishinda kwa kutumia makosa yetu nasi pia tunapaswa tushinde mchezo wetu wa marudio.

"Wachezaji wetu wapo vizuri hasa ndani ya uwanja ila walifanya makosa ambayo wapinzani wetu waliyatumia, kazi yetu ni moja kupata matokeo ili tusonge mbele katika hatua inayofuata," alisema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic