December 26, 2018


Na George Mganga

Mchezaji mkongwe aliye na rekodi ya kufunga mabao matatu pekee katika mechi dhidi ya watani wa jadi Yanga miaka ya nyuma, Abdallah Kibadeni, amelitaka benchi la ufundi la Simba kufanya marekebisho kwenye safu ya ulinzi.

Kwa mujibu wa radio One, Kibadeni amesema ni wakati mwafaka wa benchi hilo kufanya maujanja ili kukifanya kikosi kiwe kamili kutokana na madhaifu ambayo yanaoneshwa na beki hiyo.

Mkongwe huyo ameeleza hayo baada ya kuona mapungufu hayo kwa mechi za hivi karibuni haswa kwenye michezo ya kimataifa ikiwemo wa mwisho dhidi ya Nkana Red Devils ya Zambia.

Katika mechi hiyo Kibadeni ameeleza bado safu ya ulinzi haijakomaa vizuri jambo ambalo linapelekea kupata shida pale wanaposhambuliwa na wapinzani.

"Katika safu ya ulinzi ya Simba bado kuna madhaifu mengi, ni muda mwafaka wa benchi la ufundi kuangalia namna ya kurekebisha tatizo hilo ili kutoleta hatari ya kuruhusu mabao haswa katika mashindano ya kimataifa" alisema Kibadeni.

6 COMMENTS:

  1. Kama mtaalam nilifikiri angeyataja madhaifu kuliko kuzungumzia kiujumla jumla

    ReplyDelete
  2. Au ataje weak link(s), ametoa maoni ya jumla mno!

    ReplyDelete
  3. Nakubaliana naye 100% wanatengeneza line defence ambapo mabeki wote wa kati hawana mbio

    ReplyDelete
  4. Nakuunga mkono King na usinyamaze pale unapoona uzi umeregea pahala fulani

    ReplyDelete
  5. Kuna mapungufu ni lazima kushughulika nayo

    ReplyDelete
  6. SIMBA licha ya kusaka kocha msaidizi watizame kama kuna uwezkano wa kumjumuisha King kibadeni kwenye benchi la ufundi awe miongoni wa washauri wa karibu wa kocha kama wataafikiana na kocha wao baada ya kumshauri. Hatua walioingia Simba sio ya mchezo mchezo kutokana na kuwa na karibu ya klabu vigogo vyote vya soka la Africa sasa sio mbaya kuliongezea nyama benchi lao la ufundi simba kwa kocha kocha kama kibadeni aliekwishaifikisha Simba kwenye fainali ya moja ya makombe makubwa kwa ngazi za vilabu barani Africa na akaonja machungu ya kulikosa kombe hilo kwenye mchezo wa fainali. Kazi ya kibadeni kwenye benchi la ufundi iwe wazi kabisa ni kama mzee wa timu mwenye uzoefu na mashindano na wachezaji wetu wa ndani ni kumshauri mwalimu inapohitajika full stop. Nafasi ya Kocha msaidizi atafutwe kocha kijana myama asilimia 100% apate uzoefu ajekuwa kocha wa baadae.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic