December 25, 2018


Kipa wa Yanga, Mkongomani, Klaus Kindoki, jana aligeuka kuwa almasi kwa mashabiki wengi wa Yanga kumshangilia kutokana na uwezi aliouonesha uwanjani dhidi ya Tukuyu Stars.

Katika mchezo huo uliokuwa wa Kombe la FA, Kindoki alifanya vema kwa kucheza michomo kadhaa kutoka kwa wapinzani ambao walikuwa wakisakama lango lake.

Mashabiki Yanga waliamua kumpigia shangwe la maana juu ya jitihada zake licha ya siku za mwanzo kuonekana kama kituko langoni na akikosa kuaminika kwa makosa kadhaa aliyofanya.

Mashuti aliyoyachomoa jana yaliweezesha Yanga kumaliza mechi bila kuruhusu bao upande wao huku ikifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic