December 25, 2018


Straika hatari wa Yanga, Mrundi, Amis Tambwe, jana ameandika historia katika michuano ya Kombe la FA kwa kufunga mabao matatu 'hat-trick'.

Rekodi hiyo imekuwa ya tatu katika mashindano ya Kombe la FA tangu yaanze msimu huu kwani tayari mipira miwili ilikuwa imetolewa na kwenye mashindano ya FA.

Tambwe ambaye hivi karibuni alikuwa hapewi nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha Yanga jana alikuwa lulu kwa kuing'arisha Yanga dhidi ya Tukuyu Stars ikiwa ni mara yake ya kwanza kuondoka na mpira kwenye michuano hiyo ya FA.

Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, iliwakosha Yanga kuelekea sikukuu ya Krimasi leo huku akiondoka na mpira kutokana na mabao aliyofunga.

Bao jingine la Yanga kwenye kipute hicho kilichowapa safari ya kwaheri Tukuyu Stars, lilifungwa na Heritier Makambo.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic