December 5, 2018


 Baada ya kushindwa mchezo wao dhidi ya Yanga kwa kufungwa bao 3-1 licha ya kutangulia kufunga bao, kocha mkuu wa Tanzania Prisons, Mohamed Abdalah amesema  mpango mkubwa kwa sasa ni kuweza kusuka kikosi upya ili kufanya vizuri katika michezo inayofuata ya Ligi Kuu.

Prisons wamekuwa wana mwendo wa kusuasua msimu huu kutokana na kushika nafasi ya 19 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 15 na pointi kujikusanyia pointi 10.

Abdalah amesema kipindi wanachopitia kwa sasa ni mpito imani yake mambo yatakuwa sawa kwani ligi bado inaendelea.

"Matokeo ambayo tunayapata hayaleti afya kwetu sote hivyo mkakati wetu namba moja ni kuona kwamba tunajitoa hapa tulipo na kurejea kwenye ubora wetu katika ligi kuu.

"Bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na tumeshaona sehemu ambazo zinamatatizo hivyo tupo kwenye mazungumzo na baadhi ya wachezaji ili kuongeza nguvu kwenye kikosi," alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic