December 5, 2018

Uongozi wa Azam FC kupitia kwa Mratibu wake, Philip Alando umesema kuwa baada ya kumaliza kazi ya kuchukua pointi tatu kwa Stand United jana katika uwanja wa Chamazi, akili zao wanahamishia kwenye mchezo wao ujao dhidi ya Mbao FC.

Stand United walifanikiwa kuanza kuifunga Azam FC kipindi cha pili dakika ya 53 kupitia kwa Hafidhi Musa na wakashindwa kulinda ushindi huo kwa kuruhusu mabao 3.

Mabao ya Azam FC yalifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Enock Atta na bao la pili lilifungwa na Yahya Zayd kwa mkwaju wa penati kabla ya kufunga bao la tatu dakika ya 85.

Matokeo hayo yanaifanya Azam FC kufikisha pointi 36 wakiwa nafasi ya pili wakiachwa kwa pointi 2 na Yanga ambao wana pointi 38 wakiwa wamecheza wote michezo 14.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic