Baada ya Serengeti Boys kuwa kundi A lenye timu kama Angola, Uganda na Nigeria katika michuano ya Afcon U17, itakayofanyika Aprili mwakani na Tanzania wakiwa ni wenyeji, Kocha Mkuu Oscar Milambo amewatoa hofu mashabiki.
Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ilihudhuliwa na wawakilishi mbalimbali kutoka Shirikisho la Soka Afrika ‘Caf’, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt, Harrison Mwakyembe, viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’, wakiongozwa na Rais Walles Karia.
"Tuna muda wa kujiaandaa kwa ajili ya michuano hiyo, hakuna haja ya kuwa na hofu kwa kuwa ulimwengu wa sasa ni sayansi hata mpira nao pia ni sayansi, tuna nafasi ya kufanya vizuri," alisema Milambo.
Serengeti wataumana na Uganda katika kundi A, ambalo linazijumuisha timu za vijana za Nigeria na Angola, wakati katika kundi B, linazikutanisha timu za mataifa ya Guinea, Cameroon, Morocco na Senegal.
0 COMMENTS:
Post a Comment