December 7, 2018


Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, ametoa baraka zake zote kuelekea uchaguzi mkuu wa Yanga utakaofanyika Januari 13 2019.

Akilimali ambaye alikuwa sambamba na Baraza la Wazee wa Yanga, amesema wapo wapo tayari kuelekea uchaguzi huo ambao utakuwa ni wa kujaza nafasi zilizoachwa wazi ili kuwapata mbadala wao.

Aidha, Akilimali amepingana na suala la mkutano mkuu wa dharura Yanga kufanyika akiamini italeta uchonganishi kwa Baraza la Michezo nchini (BM), Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na serikali kwa ujumla.

Kutokana na kuukataa mkutano huo, Akilimali ameshauri ni vema zaidi Yanga ikazidi kuweka nguvu zake kuelekea uchaguzi mkuu pekee ambao utakuwa na manufaa kwa klabu.

"Kufanya mkutano mkuu ni uchochezi kwa serikali, BMT, TFF maana italeta uvunjifu wa amani na uchochezi kwa serikali yetu. 

Hatuna budu kutoa onyo kwa wajumbe wetu watatu waliobaki kuwa kuendelea kukaidi maagizo ya serikali, ni kuonesha utovu wa nidhamu mbele yake" alisema.

3 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Huyo ndiye mzee Akilitele anayeipenda sana Yanga. Hivi uchaguzi wa Baraza la Wazee Yanga utafanyika lini au Mzee Akilimali ni Mwenyekiti wa milele?

    ReplyDelete
  3. Mbn habari zako Mara nyingi zinazoihusu Yanga ni zilizotolewa na Akilimali ama za kuichafua tu kwani Yanga wamekunyima nn au bado unatumika kuivuruga club ya Yanga,acha mambo hayo pamoja na kwamba tunakufahamu ww ni mpenzi was Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic