December 7, 2018


Beki Mtanzania anayeichezea Nkana FC ya Zambia, Hassan Kessy amesema hana hofu kabisa mara watakapokutana na Simba kutokana  na kuzijua mbinu zao huku akiwatumia salamu viungo wachezaji Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.

Timu hizo zinatarajiwa kuvaana Desemba 14 mwaka huu mchezo utakaopigwa nchini Zambia kabla ya kurudiana kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Desemba 21 mwaka huu.


Kessy amesema kuwa hakuna mchezaji asiyemjua kwenye kikosi cha Simba, huku akiwa na matarajio makubwa ya kuwaondoa katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.


"Nusu ya wachezaji wote nimecheza nao ni wachache ambao sijacheza nao lakini wengi wao wananifahamu mimi na ninawafahamu vizuri wakiwemo hao akina Okwi na Kichuya nitakaokutana nao katika nafasi ninayocheza," alisema.


Simba wakifanikiwa kushinda katika mchezo huu wa hatua ya kwanza watajiweka katika  nafasi nzuri ya kutinga kwenye hatua ya makundi kwa kuwa mchezo wa pili wa marudiano utapigwa uwanja wa nyumbani.

3 COMMENTS:

  1. Sasa na wenyewe si wanakufahamu tatizo nini cheza Mpira acha makelele

    ReplyDelete
  2. Unawafahamu tu lakini hata ulipokuwa hapa ulikuwa unashindwa kuwazuia, kama ungeweza kuwazuia msimu uliopita ulicheza ukiwa Yanga na ukaruhusu kufungwa mzunguko wa pili. Huko kwenyewe sidhani kama namba unapata! wewe tulia tu ugali ukukute mezani, ndo utajua ni wa moto au kiporo!.

    ReplyDelete
  3. tunakujua wewe maneno mengi tena tunategemea kupata penati kupitia kwako kwa sababu ya rafu za kijinga tutakufanya Nkana wakutimue

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic