December 25, 2018


Mshambuliaji wa timu ya Simba, Emmanuel Okwi ambaye alikuwa kwenye kikosi kilichofanikiwa kuvunja rekodi ya mwaka 2003 kwa kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika amewashukuru mashabiki kwa sapoti na kuwatumia neno la sikukuu.

Simba ilifanikiwa kuitoa Nkana FC ya Zambia kwa jumla ya mabao 4-3 kwa kuwa mchezo wa kwanza ugenini walikubali kipigo cha bao 2-1 na walifanikiwa kupindua nyumbani kwa kushinda mabao 3-1.

"Mashabiki wana nguvu sana na tumefanya juhudi kwa ajili yao tunawashukuru kwa kuwa nasi bega kwa bega, ilikuwa ni muhimu kwetu kuweka historia na tumefanikiwa, Mungu awabariki na kheri ya Christmas," alisema.

Leo pia ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake Okwi ambaye ni mfungaji bora wa msimu uliopita baada ya kufanikiwa kufunga mabao 20, kwa sasa ana mabao 7 Ligi kuu na bao 1 kimataifa alilowafunga Mbabane Swallow ya Eswatin.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic