Inatajwa kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika, muda wowote kuanzia sasa, anaweza kujiuzulu katika nafasi yake hiyo kufuatia lawama anazopewa kutokana na klabu hiyo kushindwa kuwasajili nyota kadhaa ambao alikuwa anawahitaji kocha Mwinyi Zahera.
Kabla ya dirisha la usajili kufungwa Jumamosi iliyopita, Yanga ilikuwa inazifukuzia saini za wachezaji kadhaa ambao walikuwa wanawataka kuwasajili lakini waliambulia kuwapata wawili tu, Haruna Moshi ‘Boban’ na kipa Ibrahim Hamad.
Kwa mujibu wa Championi, Yanga ilikuwa inawataka wachezaji Kenny Ally, Reuben Bomba, Umar Kasumba (kutoka Kenya) na Charles Ilanfya ambao wote hao wameshindwa kujiunga na timu hiyo.
Taarifa zisizo na shaka ambazo Championi, limezipata ni kwamba Nyika amefikia uamuzi huo wa kutaka kujing’oa katika nafasi yake kutokana na lawama ambazo anazipata kutoka kwa wanachama mbalimbali kwa sababu ya kuwakosa wachezaji hao.
“Kwa sasa yeye Nyika anataka kujiweka kando kwa sababu ya kupokea lawama kutoka kwa mashabiki, hasa baada ya yale maneno ambayo aliyaongea Zahera kufuatia kutosajiliwa kwa wachezaji ambao yeye aliwapendekeza.
“Lakini hata ile ishu ya Ilanfya kilichofanya asisajiliwe ni kutokana na meneja wake kuchukua fedha za KMC ila siku mbili kabla ya usajili kufungwa, yeye alimfuata pale Pretoria Hoteli, lakini meneja wake akasema apewe muda, baadaye ndiyo ikaja kuonekana amesajiliwa KMC.
“Sasa kutokana na lawama hizo zinazoendelea, Nyika anataka kuachia ngazi na anaweza kufanya hivyo siku yoyote kuanzia kesho (leo) Ijumaa,” kilisema chanzo hicho.
Nyika altafutwa ili kufahamu juu ya hilo ambapo alisema: “Samahani kwa sasa niko sehemu nina kikao na watu, siwezi kuongea kitu, mpigie katibu (Kaimu Katibu, Omary Kaya) yeye yuko na timu ila mimi siwezi kuzungumza kitu chochote.”
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Asante
BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Aondoke huyo mzee wa 10% hana lolote zaidi ya kuihujumu team.
ReplyDeleteNYIKA kwa kika mchezaji ana% zake ndio maana HAFAI aondoke tuuu MWIZI huyo
ReplyDelete