December 22, 2018


Wakati wapenzi na mashabiki wa Yanga wakiwa na shauku kubwa ya kutaka kumuona uwanjani mchezaji wao mpya, Haruna Moshi ‘Boban’, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linadaiwa kumzuia mchezaji huyo kuitumikia timu hiyo.

Boban alijiunga na Yanga hivi karibuni katika dirisha dogo la usajili akitokea African Lyon ambayo pia aliungana nayo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Friends Rangers inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Meneja wa Boban, Herry Mzozo, alisema TFF imemzuia Boban kuitumikia Yanga kutokana na maagizo yake iliyoyatoa hivi karibuni kwa timu zote za ligi kuu kuto­watumia wachezaji wa ndani waliosajiliwa katika dirisha dogo la usajili mpaka hapo Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji itakapokutana na kupitia usajili huo.

Alisema kama isingekuwa hivyo, basi Boban angeanza kuitumikia Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wa Jumapili iliyopita ambao timu hiyo iliibuka na ushindi wa mabao 3-2 lakini hakuweza kuonekana uwanjani kutokana na maagizo hayo ya TFF.

“Hiyo ndiyo sababu kubwa hasa ambayo imemfanya Boban mpaka sasa ashindwe kuitumikia Yanga japokuwa tayari al­ishajiunga nayo kwa ajili ya mazoezi.

“Hata hivyo, ngoja tuendelee kuisubiri kamati hiyo mpaka hapo itakapokutana na kutoa maamuzi,” alisema Mzozo.

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS
Kwa wasomaji wa Blog yetu pendwa ya michezo hakikisha una nifollow INSTAGRAM kwa kubonyeza link iliyopo hapo Juu tutakudodoshea Upates zote za michezo kuanzia sasa.
Asante

BONYEZA HAPA ===> SALEH JEMBE SPORTS

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic