December 5, 2018



 
Timu ya Yanga ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa winga wa Singida United, Tiber John katika kuimarisha kikosi chao wakati wa dirisha dogo la usajili linalokaribia kufungwa.

Usajili wa dirisha dogo ulifunguliwa Novemba 15 na utafungwa Desemba 15 mwaka huu na Yanga ipo kwenye mazungumzo ya mwisho kumsajili beki wa Lipuli, Ally Mtoni, Eliud Ambokile (Mbeya City) Vitalis Mayanga (Ndanda) Keny Ally (Singida United) na winga kutoka Congo, Reuben Bomba ambaye yupo nchini.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa Yanga inataka kuimarisha kikosi chake kuelekea kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.

"Wakati wowote Tiber atasaini mkataba kuchezea timu ya Yanga katika usajili wa dirisha dogo ni baada ya viongozi kuanza kufanya naye mazungumzo kilichokuwa kinachelewesha ni mechi dhidi ya Prisons viongozi walikuwa kwenye maandalizi na kusababisha kusitisha baadhi ya vitu likiwemo usajili," kilieleza.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Yanga, Hussen Nyika alisema kuwa muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa kuhusu usajili wa Yanga.

"Wiki hii ndio tunaanza usajili rasmi wa wachezaji wapya katika dirisha dogo, hivyo ni vigumu kumtaja moja kwa moja Tiber, tusubiri muda ukifika tutaweka wazi," alisema.

Kutoka Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic