December 5, 2018


Baada ya juzi jumatatu, Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Prisons ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, mashabiki wa Yanga walifanya uharibifu uwanjani.

Mashabiki hao waliharibu fensi inayotenganisha sehemu ya mashabiki na uwanja baada ya kuingia uwanjani na kuanza kushangilia ushindi huo mara tu mchezo ulipomalizika.

Meneja wa Uwanja huo, Modestus Mwaluka, alisema kutokana na kitendo hicho anawaandikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) barua ya malalamiko juu ya uharibifu.

"Kitendo hicho ambacho kimefanywa na mashabiki wa Yanga siyo cha kimichezo, hivyo nawaandikia barua TFF ili wao ndiyo wajue watawachukulia hatua gani," alisema.

Kutoka Championi

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic