December 1, 2018


Kocha Mkuu wa Yan­ga, Mwinyi Zahera raia wa DR Congo amewe­ka wazi kwamba ana­muamini straika wake, Heriti­er Makambo kuwa ana uwezo wa kufunga zaidi ya mabao 16 kwenye ligi kutokana na kufunga idadi hiyo kwenye ligi ngumu ya Congo.

Makambo ana mabao saba sambamba na washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Em­manuel Okwi .

Zahera amesema kwamba anamuamini kwa saba­bu tayari alishafanya naye kazi nchini Congo na alifunga mabao mengi akipambana na timu kama TP Mazembe, hivyo hawezi kushindwa kufunga katika ligi ya Tanzania kutokana na kutoku­wepo ugumu sana kulinganisha na huko.

“Wakati ambao Makambo hakuwa anafunga mashabiki wakaanza kuongea lakini ni­waambie kwamba hilo suala siyo ishu kwake kwa sababu nime­fanya naye kazi DR Congo ali­wahi kufunga mabao 16 kwenye mechi nane za ligi.


“Kwenye suala la kufunga ninamuamini kwamba hatani­angusha na niwaambie kwamba atafunga zaidi, ni suala la ku­pewa muda tu,” alisema Zahera.

6 COMMENTS:

  1. Lakini sasa kwa tunavyowajua TP Mazembe kwa kupenda vilivyo bora katika suala la kutafuta wachezaji wenye uwezo vipi washindwe kumuona makambo kama kweli ni mchezaji mwenye uwezo? Na vipi makambo anakubali kushinda na njaa pale yanga wakati hata mtibwa ingempeleka kimataifa na asingeasirika kisaikojia kutokana na migomo ya wachezaji pale yanga. Ligi bado mbichi tena sana kwa hivyo wacha tuone nini kitatokea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana na coach kuwa makambo ni mshamuliaji mzuri ukifananisha na wengine kwa kigezo kimoja tu...makambo amejitahidi kufunga magoli yote saba ktk mechi tofauti kila goli lkn wengine wamefunga goli mbili mbili ktk mechi rahisi lkn mikoani wameshindwa kufunga...ligi bado ndefu tutaelewana tu

      Delete
    2. Nikweli makambo amejidhihirisha kwamba nimshambuliaji mzuri ukiangalia hata aina yamagolianayofunga,napingana nahoja kwamba makambo kama mzuri kwanini asingeenda tp mazembe hiyo nihoja dhaifu sana kwanihata kule Kongo sio kila mchezaji.mzuri anacheza tp mazembe zipo timu nyingi.mzuri.pale kuna As vita,motema pembe.nazo zina mastaa

      Delete
    3. Nikweli makambo amejidhihirisha kwamba nimshambuliaji mzuri ukiangalia hata aina yayamagolianayofunga,napingana nahoja kwamba makambo kama mzuri kwanini asingeenda tp mazembe hiyo nihoja dhaifu sana kwanihata kule Kongo sio kila mchezaji.mzuri anacheza tp mazembe zipo timu nyingi.mzuri.pale kuna As vita,motema pembe.nazo zina mastaa

      Delete
  2. Sasa hapo kiboko ya simba ndo nan??? huu ni ujinga wa kiwango cha phd

    ReplyDelete
  3. So mama Zahera haji tena kuichezea Yanga?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic