Mtanzania Abdi Banda anayeichezea Baroka FC ya mjini Polokwane atakutana kwa mara ya kwanza na kikosi cha kocha wake wa zamani, Dyran Kerr katika mechi ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, leo.
Kerr anainoa Black Leopards ya Polokwane nchini Afrika Kusini wakati Banda anaichezea Baroka na timu hizo zina upinzani mkubwa na kufanya Polokwane Derby kuwa moto.
Banda ameiambia SALEHJEMBE kwamba wamejiandaa vizuri na wanajua itakuwa ni mechi ngumu na gumzo.
“Tumejiandaa, najua nakutana na Kocha Kerr kwa mara ya kwanza. Matumaini makubwa ni kushinda lakini najua haitakuwa kazi lahisi,” alisema kutoka mjini Polokwane.
Kabla, Kerr na Banda walikuwa pamoja katika kikosi cha Simba, lakini Kerr raia wa England alianza kutimuliwa na kwenda kuinoa Gor Mahia ya Kenya na baadaye Banda aliondoka na kujiunga na Baroka FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment