January 6, 2019


NAHODHA na Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu amekuwa ni kinara wa kutoa pasi za mwisho za mabao katika michezo ya Yanga waliyocheza Ligi Kuu Bara.

Yanga ina jumla ya mabao 35 iliyofunga kwa sasa kwenye ligi na imefanikiwa kukusanya jumla ya pointi 50.

Rekodi ya pasi za  mabao ya Ajibu msimu huu ipo namna hii katika michezo ambayo wamecheza pamoja na wafungaji wake wa mabao kama ifuatavyo:-

1. Yanga na Stand United
Katika mchezo huu Ajibu uliochezwa Uwanja wa Taifa, Yanga ilisha maba 4-3, alitoa pasi tatu za mabao na ni mchezo huu alitoa pasi nyingi zaidi kwenye ligi mpaka sasa.

Wafungaji walikuwa ni Mrisho Ngassa dakika ya kwanza ambayo haijafikiwa mpaka sasa ndani ya Yanga, Andrew Vincet 'Dante'  na Deus Kaseke akimalizia pasi ya kichwa aliyoipokea kutoka kwa Ajibu.

2.Yanga na Ndanda

Mchezo Ajibu uliisaidia Yanga walitanguliwa kufungwa na Ndanda katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa na kukubali sare ya kufungana bao 1-1.

Ajibu alitoa assist moja kwa njia ya faulo iliyotendewa haki na kiungo mshambuliaji chipukizi Jaffary Mohammed aliyefunga bao lake la kwanza ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kwa kichwa.

3.Yanga na Coastal Union

Mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Taifa, Ajibu alihusika kwa kumtengenezea pasi ya bao moja aliyoitoa moja kwa moja kwa mguu wake wa kulia na ikapokelewa kwa mguu wa kulia na Makambo akafunga bao.

4.Yanga na Singida United

Wengi walikuwa wameanza kumsahau Ammis Tambwe, Ajibu alimuibua katika mchezo huu ambao Yanga ilishinda kwa mabao 2, Uwanja wa Taifa. Ajibu alimpa pasi Tambwe akafunga bao la ushindi.

5.Yanga na Aliance School

Pasi mbili alizitengeneza Ajibu kwa wachezaji wawili tofauti kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa na Yanga ilishinda kwa mabao 3-0. Ajibu alimpa pasi ya bao Makambo na Mrisho Ngassa.

6.Yanga na Mbao

 Kwenye mchezo huu uliochezwa Uwanja wa Taifa Yanga ilishinda bao 2-0, Ajibu alimpa pasi ya bao Rafael Daud


7.Yanga na Tanzania  Prisons

Kwenye mchezo huu Ajibu alitoa pasi moja ya bao Tambwe ambaye alifunga bao la tatu na kuwafanya wapinzani wao wasiamini kilichowakuta kwani walifungwa jumla ya mabao 3-1 wakiwa nyumbani, Uwanja wa Sokoine Mbeya.

8.Yanga na Ruvu Shooting

Katika mchezo huu Ajibu alitoa pasi moja ya bao  lilifungwa na Makambo, Yanga ilishinda kwa mabao 3-2 Uwanja wa Taifa.

9.Yanga na African Lyon

Mchezo huu Ajibu alitengeneza pasi moja ya bao kwa mpira wa faulo iliyomfikia Abdalah Shaibu 'Ninja' aliyefunga kwa kichwa na kuisaidia Yanga kubeba pointi tatu katika mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

10.Yanga na Mbeya City

Kwenye mchezo huu uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Ajibu alitoa pasi moja ya bao baada ya kupiga faulo ambayo ilimfikia Makambo akamalizia kwa kuipeleka kimiani na kuisadia Yanga kubeba pointi tatu na ulikuwa ni mchezo wao wa kufungia mwaka walishinda mabao 2-1.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic