NAHODHA wa Simba, John Bocco leo ameongoza msafara wa kikosi cha Simba ambacho kimeanza safari yake kuelekea nchini Misri kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaochezwa Februari 2.
Bocco alikuwa nje kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha ambayo aliyapata katika mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura na aliwakosa AS Vita wa Congo ila kwa leo amejiunga na timu ili kuongeza morali ndani ya kikosi hicho.
Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema wachezaji wote wameandaliwa kisaikolojia na wanakwenda kwa tahadhari kuwavaa waarabu hao kwa kuwa ni timu bora.
"Tunakwenda kucheza na timu bora ila tutaingia kwa tahadhari kubwa na lengo letu litakuwa ni kushambulia na kujilinda kwani tukisema tujilinde muda wote itakuwa hatari kwenye lango letu.
"Uwepo wa Bocco ndani ya kikosi chetu unaongeza nguvu kwani wachezaji wangu wote siku zote huwa nasema wana uwezo mkubwa ila wanasumbuliwa na tatizo la kukosa umakini wakiwa eneo la hatari imani yangu tatizo litatapata tiba," alisema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment