January 27, 2019


Yanga wana kibarua kigumu cha kupambana kwenye Ligi Kuu Bara kwa mwezi ujao wa Februari kutokana na ratiba yao kuonyesha wana mzigo wa mechi tano mfululizo ambao watazicheza ndani ya siku 17 tu.

Yanga wanaofundishwa na Kocha Mwinyi Zahera raia wa DR Congo, watakabiliana na dakika 450 ngumu katika mwezi huo baada ya ratiba mpya yenye viporo kuanikwa Jumatatu iliyopita na Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB).

Timu hiyo ambayo kwa sasa ina pointi 53 katika ligi hiyo ikiwa ndiyo inaongoza, katika mechi hizo za mwezi ujao, tatu mfululizo watacheza ugenini, kisha moja nyumbani, baadaye wataenda ugenini tena.

Ratiba ya Yanga inasoma hivi; Februari 3 watakipiga na Coastal Union mkoani Tanga, Februari 6 dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua uliopo mkoani Singida, kisha Februari 10 watakuwa mkoani Tanga kucheza na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Baada ya mechi hizo tatu mfululizo za mkoani, Februari 16 watacheza dhidi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kisha watasafiri kuelekea Mwanza kucheza na Mbao FC Februari 20 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba. 

Hesabu zinaonyesha kwamba Yanga watatumia siku 17 kucheza mechi hizo tano huku wakipumzika kwa siku tatu hadi nne kabla ya mechi nyingine.

Yanga watapumzika siku mbili baada ya kumaliza mechi na Coastal kucheza na Singida kisha siku tatu kabla ya mechi na JKT Tanzania. Watakaa kwa siku tano kuvuta pumzi ya kuwawinda Simba, Februari 20 kabla ya siku nne mbele kwenda Mwanza.

2 COMMENTS:

  1. Mazingira yale yale kama ya mwaka jana, kupangiwa mechi mfululizo wakati unaoenda kucheza nao wamepumnzika,

    ReplyDelete
  2. mechi zimepangwa hivi ili kuidhoofisha Yanga na kuisaidia simba ichukue ubingwa ligi kuu TFF Mungu anaowaona

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic