January 27, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameweka wazi kuwa hafurahishwi na maneno ya wadau wa soka kuhusu uwezo wa Klaus Kindoki na kwamba hata kama angekuwepo Beno Kakolanya golini basi naye angefungwa tu.

Wadau mbalimbali wa soka nchini wamekuwa wakiponda kiwango cha kipa Kindoki kutokana na mabao anayofungwa wakidai ni mepesi hivyo wameshauri Kakolanya ambaye aliondolewa na Zahera arejeshwe haraka kuokoa jahazi. 

Shutuma hizo zilijitokeza kwenye mechi dhidi ya Stand United ambapo Yanga ilifungwa bao 1-0 ikiwa ni mechi ya ligi kisha hivi karibuni ikafungwa tena na Kariobangi Sharks ya Kenya kwa mabao 3-2.

Kutokana na shutuma hizo, Zahera ameliambia Championi Jumamosi kuwa, hafurahishwi na suala la kuambiwa amtafute Kakolanya ili wazungumze juu ya kumrejesha Yanga wakati ishu iko wazi kuwa yeye mwenyewe ndiye aliamua kuondoka Yanga bila ruhusa ya kiongozi yeyote.

“Mashabiki wa mpira wasipende kunishinikiza mimi kumtafuta Kakolanya wakati yeye mwenyewe anajua wajibu wake pale anapokuwa amekosea, Yanga ina uongozi ambao unafuata misingi na taratibu za soka hivyo kama kuna jambo ambalo wanadhani mimi sijalifanikisha hadi awepo Kakolanya basi wafuate taratibu zinazostahili na si kuhusisha matokeo na ishu hiyo.

“Mashabiki wazuri wa Yanga wanatakiwa kuamini kuwa kila mchezaji aliyepo kikosini anafaa kuitumikia timu bila kuwaza pengo lolote kwani nia yetu siku zote ni ushindi na tutaendelea kushinda maana kufungwa nayo ni sehemu ya mchezo tu,” alisema Zahera.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic