January 28, 2019


Kipigo cha mabao 2-1 walichokipata kutoka kwa Bandari juzi kiliwatokea puani baada ya jana Kocha Patrick Aussems kuwaanika juani kwa zaidi ya dakika 60 walipokuwa na kikao kizito kilichofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

Katika kikao hicho kilichoanza kabla ya mazoezi, Aussems alitumia muda huo kuwakumbusha wachezaji hao majukumu yao ambayo wanapaswa kuifanyia Simba katika kipindi hiki ambacho inakabiliwa mi mechi nyingi ngumu.

Mmoja wa wachezaji wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini aliliambia Spoti Xtra kuwa: “Mbali na kutukumbusha majukumu yetu lakini pia kocha alizungumzia kuhusiana na kiwango kibovu tulichoonyesha tulipocheza na Bandari juzi Ijumaa.”

“Alisema hakufurahishwa kabisa na uwezo wetu tulioonyesha katika mechi hiyo, kwa hiyo ametutaka tujitambue na kuachana na tabia ya kuweka mbele starehe kuliko kazi.

Katika hatua nyingine, msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amewaomba radhi mashabiki kufuatia kutolewa kwa timu yao kwenye michuano ya Sportpesa.

Manara alisema wanaelewa fika kuwa mashabiki wameumizwa na kutolewa huko kwa timu yao kwa hiyo amewaomba watulie huku kocha akirekebisha makosa ili wafanye vizuri kwenye Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

2 COMMENTS:

  1. Uongozi wa #Simba unapaswa kujitambua nini wanataka ili waweze kuwabana zaidi wachezaji..
    Kama uongozi wa juu haujitambui itakuwa ni shida sana..
    Cha kusikitisha ni kuwa wanadiriki kuendelee kutumia mashindano yenye ushindani mkubwa kama sehemu ya majaribio..!!
    Kuna wakati ikibidi kuchukua maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya timu wayachukue bila kuangalia nyuma..

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana, kusikia kwamba kambini timu anaachiwa kocha peke yake! Mnatupeleka wapi jamani na hii timu yetu! Au labda sisi washabiki na wapenzi wa timu ndio tunaoujua sana umuhimu wa kombe la S/PESA kuliko uongozi wa timu?

    Meneja wa timu kazi yake ni nini hadi aachwe kocha peke yake kambini!

    Hivi mpira au kiwango kilionyweshwa jana na Timu dhidi ya Mbao kama kingeonyeshwa kwa Bandari, si goli 5 tungewapiga wale! Sasa kwanini mnapenda kuleta masihala kwenye mashindano?

    Iwapo mnaona mashindano fulani hayana umuhimu kwenu, uongozi muwe mnaitoa timu kwenye mashindano hayo pindi tyu mnapoalikwa au mnapopata taarifa ya mashindano hayo.

    Maana inapofikia hatua mnadharau mashindano eti kisa mnashiriki mashindano makubwa ya Afrika, matokeo yake ndio haya ya kufungwa na vitimu ambavyo havina mafanikio yoyote hapa Afrika Mashariki.

    Na katika hili, nadhani hamkujifunza na yaliyotokea katika fainali ya Mapinduzi, mkatupelekea akina Muzamiru, akina Salamba matokeo yake mkayaona. Kwa kisingizio eti timu inajiandaa na mechi ya Klabu bingwa Afrika!, na bado hiyo timu iliyokaa pembeni ikaenda kupigwa goli 5! Kipi bora hapo sasa!.

    Kama mnepeleka timu inayoeleweka Zanzibar kuchukua kombe la Mapinduzi, ina maana Congo tungefungwa goli 10?, maana hapo sasa mantiki yake kujiandaa kule kwa timu kumepunguza idadi ya magoli!.

    Sasa cha ajabu Kombe la Mapinduzi tumelipoteza na bado goli 5 tumepigwa!.

    Menejimenti ijitathimini. Uongozi wa Mpira sio sawa na uongozi wa familia za nyumbani zenye watoto wa3 hadi wa5. Mpira ukiwashinda, mkabaki kuongoza familia zenu tu, muwaachie wanaoweza kuongoza mpira. Matokeo yake mnamlete mzigo mtu mmoja tu hapo ambaye anaifanya kazi yake kwa weledi na kutimiza majukumu yake, Bwana Manara anatukanwa bila sababu za msingi! Huku ninyi mpo kimya mnakuna matumbo tu!. MNATUUMIZA MASHABIKI BWANA!.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic