January 6, 2019


MSHAMBULIAJI  wa timu ya Yanga, Heritier Makambo amekuwa mchezaji wa kwanza msimu huu kuweka rekodi ya aina yake baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo.

Makambo amefanikiwa kufanya hivyo mfululizo ikiwa ni baada ya kupokea tuzo hiyo mara ya kwanza mwezi Novemba akiwashinda wachezaji wawili aliofika nao fainali kwenye hatua hiyo ambao ni Said Dilunga wa Ruvu Shooting na beki wa Yanga Abdalah Shaibu 'Ninja'.

Mwezi Desemba amefanikiwa kuibuka na tuzo hiyo baada ya kuwashinda wachezaji wawili aliofika nao fainali ambao ni Miraj Athumani wa Lipuli na Idd Seleman 'Nando' wa Mbeya City.

Rekodi yake inakuwa ya kwanza kwani mpaka sasa hakuna mchezaji ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara mbili mfululizo, Makambo anafanikiwa kukunja shilingi milioni mbili mfukoni ambazo ni zawadi alizopewa baada ya kushinda tuzo hizo.

Mshindi wa kwanza alikuwa ni Meddie Kagere mwezi Agosti akafuatia Eliud Ambokile mwezi Septemba, Emanuel Okwi mwezi October, Novemba na Desemba zote akakomba Makambo tuzo pamoja na kisimbusi cha Azam TV.

Kwa upande wa Kocha, Mwinyi Zahera amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo mara tatu mpaka sasa ikiwa ni mwezi Septemba, Novemba na Desemba akiwaacha mbali makocha wengine wote wa kibongo huku Patrick Aussems akiishia kuingia fainali.

Kutoka Spoti Xtra

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic