January 6, 2019


WAPINZANI wa Simba kwenye hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika, wanazidi kuonyesha kwamba wanaweza kufungika endapo Simba watachanga karata vema kwani wanaonekana ni wepesi kufungwa na kasi yao ni kipindi cha kwanza.

Simba inawakilisha Taifa katika hatua ya makundi ikiwa kundi D ambalo lina timu kama JS Saoura ya Algeria, AS Vita ya Congo na Al Ahly ya Misri ambayo ina historia ya kuzisumbua timu kubwa kutoka Tanzania.

JS Saoura ya Algeria ambayo mtanzania Thomas Ulimwengu anaichezea itakuwa timu ya kwanza kucheza na Simba, Januari 12 Uwanja wa Taifa, juzi ilipokea kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wao wa Ligi dhidi ya JS Kabylie.

JS Saoure inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ya Algeria ilikubali kupoteza mchezo huo wa ligi uliochezwa juzi baada ya Fiston Abdoul wa JS Kabylie kupachika bao dakika ya 52.

Al Ahly ya Misri wao wanaonekana kuwa na kasi kipindi cha kwanza wana juhudi kubwa kutafuta matokeo kwani katika mchezo wao dhidi ya Pyramids walifanikiwa kufunga bao dakika ya 33 kupitia kwa Walid Azaro ila mambo yalibadilika kipindi cha pili, wapinzani walipindua matokeo dakika ya 47 kupitia kwa Mohamed Farouk na Abdallah Said dakika ya 57.

Kutoka Spoti Xtra

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic