January 25, 2019




KIKOSI cha Bandari FC kutoka Kenya kimetinga hatua ya fainali baada ya kuifunga Simba mabao 2-1 katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliochezwa Uwanja wa Taifa leo.


Simba walikuwa wa kwanza kuandika bao kipindi cha kwanza dakika ya 45 kupitia kwa mshambuliaji Meddie Kagere ambalo lilidumu kwa muda wa mpaka dakika ya 59 ambapo Bandari walifunga bao kwa mkwaju wa Penalti lililofungwa na William Waydi.

Dakika ya 75 Bandari walifunga bao la pili kupitia kwa Wilberforce Lugogo baada ya kukutana na mpira uliotemwa na Manula na kuifanya Simba kuwa nyuma kwa bao 1.

 Kwa matokeo hayo Simba wanaishia hatua ya nusu fainali watasubiri atakayefungwa katika mchezo wa Mbao na KK Sharks kucheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu.

5 COMMENTS:

  1. This is Simba Bwana!!! Soka la Tanzania huchezewa midomoni na magazetini tutaitarajie Mbao kufanya kitu cha maana kabla ya hawa walevi wetu wa sifa.

    ReplyDelete
  2. Tunapoteza muda wetu tu.hatuna timu serious maneno mengi sana. Acha tufundishwe kuwa serious. Huu mpira wetu bado ni Mpira wa ridhaa. Tunasafari ndefu. Unajaribu timu kwenye mashindano makubwa.ushwahili umetuzidi. Acha tuone uhalisia wetu. Tuache masifa ya kijinga

    ReplyDelete
  3. mATUSI MENGI MPIRA HAKUNA,WAUZA MAJI NYIEEEE

    ReplyDelete
  4. Acha wawashwe maana wameropoka sana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic